TANZANIA
imekuwa mwenyeji wa semina ya waamuzi chipukizi barani Afrika inayoaanza leo
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Baraka
Kizuguto alisema kuwa jumla ya waamuzi 29 toka nchini wanachama wa Shirikisho
la Soka Barani Afrika (CAF) watahudhuria semiana hiyo huku Tanzania
ikiwakilishwa na waamuzi wawili.
“Semina hii
ambayo itaanza kesho (leo) ni ya waamuzi chipukizi ambao hawana beji za FIFA na
itamalizika Septemba 30”, alisema Kizuguto.
Pia Kizuguto
alisema waamuzi Shomari Lawi wa Kigoma na Abdallah Kambuzi wa Shinyanga ndio
watakaowakilisha Tanzania.
Wakati huohuo Rais wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry kufuatia vifo vya mahujaji zaidi ya
700 vilivyotokea Maka wakati wa kuhiji.Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole waislamu wote duniani kufuatia vifo vya mahujaji hao zaidi ya 700 vilivyotokea juzi na majeruhi zaidi ya 400 wakati wa ibada ya hija.
Malinzi amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini TFF inawapa pole wafiwa wote, ndugu jamaa na marafiki na kuwatakia majeruhi afya njema na kusema ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.

No comments:
Post a Comment