KUELEKEA kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania
Bara dhidi ya Yanga na Simba, Mkuu wa kitengo cha habari wa Yanga, Jerry Muro
amerusha kijembe kwa mahasimu wao.
Mchezo baina ya vigogo hao wa soka nchini
utachezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa ikiwa kila timu imeshashinda
michezo mitatu na kushinda yote.
Muro amewafananisha mahasimu wao Simba, na
kisigino ambacho daima huwa nyuma si mbele.
“Sisi si kama ‘wamchangani-Simba’ ambao
‘ kutwa’ hawaishi kuongea bila kutekeleza ila niseme wazi tumeshinda michezo
yetu yote na tunaongoza ligi, tunachokifanya sasa ni kuendelea kuwa juu
kuhakikisha tunatimiza wajibu kwani nafahamu kamwe kisigino hakiwezi kuwa mbele, siku zote
kimekuwa nyuma. Haitawahi itokee hao ‘ wamchangani’ wakakaa mbele yetu”,
alijigamba Muro
Pia alisema Yanga imejipanga vizuri hivyo
anawataarifu wapenzi na wanachama popote
pale walipo kuwa timu inaendelea vizuri na kambi ya maandalizi kuelekea mchezo wa
Jumamosi.
“Hatutakuwa kuwa wazungumzaji sana,
tunawaomba mashabiki wetu watupe muda wa kujitathimini na tuwe na wakati mzuri
wa kukitayarisha kikosi chetu ili mwisho wa siku tuweze kupata matokeo mazuri
zaidi, maneno siyo yatakayofanya kazi”, alisema Muro ambaye timu yake imeweka
kambi Pemba.
Yanga imeshinda mabao 2-0 dhidi ya Coastal
Union ya Tanga katika mchezo wa kwanza kisha wakashinda 3-0 dhidi ya Tanzania
Prisons katika mchezo wa pili, wakaifunga JKT Ruvu mabao na kufikisha alama 9
sawa na timu za Simba, Mtibwa Sugar na Azam FC ambazo pia zimeshinda michezo
yao mitatu ya mwanzo msimu huu.
Yanga wanaongoza ligi kutokana na wastani wao
mzuri wa magoli 8. Wamefunga magoli 9, wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara
moja.
Simba pia wameanza ligi kwa ushindi
mfululizo, wameshinda 1-0 dhidi ya Africans Sports, kisha wakashinda 2-0 dhidi
ya JKT Mgambo na mechi hizo zote mbili za mwanzo walichezea ugenini, Mkwakwani ,Tanga.
Mechi yao ya kwanza katika uwanja wa Taifa
msimu huu walishinda 3-1 dhidi ya Kagera Sugar FC Jumapili iliyopita
lakini hilo halimtishi, Jerry ambaye amesisitiza Yanga inahitaji utulivu na
muda zaidi kabla ya kuendeleza ushindi wao wa Jumamosi hii.
No comments:
Post a Comment