RAIS wa
Shirikisho la soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amefunga kozi ya makocha
lesseni C inayotambuliwa na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) na kuwataka
wahitimu hao kufanyia kazi mafunzo waliyoyapata.
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya kufunga mafunzo hayo, Malinzi amesema kuwa anasikitika
kuona makocha wanapata mafunzo kama hayo lakini wanaenda kuweka vyeti vyao
‘makabatini’ na kuacha kufanyia kazi walichojifunza.
“Hiki
mlichokipata kwenye mafunzo haya ya wiki mbili mnatakiwa muende mkafanyie kazi
kwa kutafuta timu za kufundisha na baada ya mwaka mmoja ni vizuri mkajiendeleza
zaidi ya hapa,” alisema Malinzi
Aidha,
amesema kuwa Shirikisho lake limepanga kuhakikisha baada ya muda litafuta
utaratibu wa makocha wenye lesseni C kuwa kwenye benchi la ufundi la timu za
daraja la kwanza na kuwa wasaidizi kwenye benchi la ufundi la timu za ligi kuu.
“kwa sasa
hivi makocha wa ligi kuu wanatakiwa kuwa na leseni ya daraja B na wasaidizi
angalau leseni daraja C, ila kuanzia msimu wa 2017-2018 mambo yatabadilika na
lessen I C aizataruhusiwa kwenye mabenchi ya ufunzi kwa timu za ligi kuu, mambo
yataendelea hivyo mpaka mwisho tutakuwa na leseni za daraja A,” alisema
Malinzi.
Aidha,
aliwataka wahitimu hao ambao wengi wao wanatoka kwenye klabu za daraja la
kwanza na wengine wakiwa makocha wasaidizi kwenye klabu za ligi kuu,
kuhakikisha wanatumia ujuzi walioupata kwenye mafunzo hayo kuzisaidia timu zao.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Chama Cha soka mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo,
ameishukuru TFF kwa jitihada za kuendeleza mchezo wa soka nchini na kuelelezea
changamoto wanazokutana nazo katika kuandaa kozi kama hizo kwa vyama vya soka
vya mikoa nchini.
“Sisi DRFA
tumefanikiwa kuendesha kozi hii kwa sababu ya uwepo wa timu za Simba, Yanga na
Azam kwenye ligi kuu ambazo ni sehemu ya mapato kwa chama chetu, ila kwa vyama
vingine hali inakuwa ngumu kuandaa na kuendesha mafunzo kama hayo,” alisema
Kasongo.
Kozi hiyo
ya wiki mbili ilikuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa TFF na kuendeshwa na mkufunzi
anayetambulika na CAF, Salum Madadi ambaye pia ni Mkurugenzi wa ufundi wa TFF
ambapo makocha 30 wamehitimu.
No comments:
Post a Comment