Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limefungua kesi kwenye
Kamati ya Nidhamu ya FIFA dhidi ya klabu ya Etoile Sportive du Saleh ya
Tunisa kutokana na klabu hiyo kushindwa kuilipa klabu ya Simba SC ya
Tanzania pesa za mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi.
Kwa mujibu wa barua ya FIFA kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la
Tunisia (FTF) na nakala yake kwenda TFF, klabu hiyo inashitakiwa kwa
kuvunja kanuni kwa mujibu wa ibara ya 64 ya kanuni za nidhamu za FIFA
(Fifa Disciplinary Code).
Kwa kuzingatia hilo, agenda hii itakuwa kwenye kikao kijacho cha kamati ya nidhamu.
Etoile Sportive du Sahel wametakiwa kulipa mara moja kiasi cha dola
za kimarekani laki 3 na riba ya asilimia 2% kwa kila mwaka kama
ilivyoelekezwa na maamuzi ya Jaji mmoja wa Kamati ya Nidhamu za
Wachezaji mnamo tarehe 20 Novemba 2014.
Tangu wakati huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekua
likiwasiliana na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Tunisia (FTF) na FIFA
kwa niaba ya klabu ya Simba amabye ni mwanachama wa TFF.
Ikiwa klabu hiyo ya Tunisia itafanya malipo kwa klabu ya Simba na
kupelekea ushahidi wa malipo kwa FIFA basi suala hilo litafutwa.
Aidha klabu hiyo iko kwenye hatari ya kushushwa daraja au kupokwa
alama kwenye ligi (League Point) iwapo haitalishughulikia suala hilo
mara moja.
No comments:
Post a Comment