Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 4, 2015

DANNY WELBECK NJE MWEZI MMOJA


straika wa Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja hadi Krismasi baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti lake.
Welbeck, mwenye Miaka 24, aliumia Goti lake mwishoni mwa Aprili baada ya kuifungia Arsenal Bao 8 katika Mechi zake 34 tangu ahamie hapo kutoka Man United. 

Klabu ya Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni.
Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikujiimarisha kwa kununua Mchezaji yoyote wa mbele mbali ya kumnunua Kipa Mkongwe kutoka Chelsea Petr Cech.

Hivi Juzi Washabiki rasmi wa Arsenal walikuja juu na kutaka uchunguzi wa haraka ufanywe kwa nini Klabu yao hainunui Wachezaji kama Klabu nyingine.

No comments:

Post a Comment