Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 6, 2015

WAKATI YANGA IKIMUONA WA KAZI GANI, KASEJA AGEUKA LULU



 KASEJA
BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumweka huru aliyekuwa  golikipa wa Yanga Juma Kaseja  klabu za Mbeya City, Mwadui FC na Ndanda FC zinapigana vikumbo kuwania saini yake.

Akizungumza jijini Kaseja amekiri kufutwa na viongozi wa klabu hizo lakini hakuweka wazi ni klabu gani ambayo atajiunga nayo akitaka mashabiki wasubiri watajua muda ukifika.

“Ni kweli nimefanya mazungumzo na viongozi wa Mbeya City kwa ajili ya kunisajili na naamini Mbeya City ni timu nzuri ambayo inaleta changamoto pia kocha wao Juma Mwambusi tunafahamaana tangu akifundisha Moro Utd, na leo (jana) timu ya Ndanda ya mkoani Mtwara imeonyesha nia ya kunisajili hivyo tunavyozungumza wakala wangu yupo nao kwenye mazungumzo”, alisema Kaseja.

Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo amekaririwa na vyombo vya habari akisema endapo mambo yatakwenda vizuri atamsajili Kaseja kwani ni kati ya magolikipa npra nchini.

TFF imemruhusu Juma Kaseja kujiunga na timu yoyote baada ya kupitia maombi yaliyoletwa kwao na Chama cha wacheza Soka Tanzania (SPUTANZA) kikiomba mchezaji huyo kuwa huru na kujiunga na klabu yoyote.

Aidha Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amethibitisha kumruhusu Kaseja kujiunga na klabu yoyote ambayo atakubaliana nayo atacheza kwa muda wote ambao suala lake la mgogoro na Yanga likiwa linashughulikiwa kwani hawajamwondoa kwenye mgogoro wa kikazi na klabu yake.

No comments:

Post a Comment