WAKATI
dirisha la usajili kwa klabu vya Ligi Kuu nchini (VPL), Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) likifungwa juzi timu vitatu vya VPL
vimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa wachezaji katika muda uliopangwa.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alivitaja Klabu za Coastal Union ya
Tanga, Stand United ya Shinyanga na Toto African ya jijini Mwanza kuwa zimeshindwa
kuwasilisha usajili wao na kusema faini ni 500,000 kwa mchezaji mmoja hivyo klabu
iliyochelewesha usajili au itakayobadili majina au kuongeza majina baada ya
usajili kufungwa italazimika kulipia faini“Usajili umefungwa jana (juzi) na timu tatu hazijawasilisha usajili wao hata wa mchezaji mmoja pamoja na TFF kuongeza muda wa usajili kwa wiki mbili”, alisema Kizunguto
Pia alisema si kwamba timu zingine zimefikisha idadi ya wachezaji wote kulingana na kanuni bali zingine zimesajili wachezaji 18, 24 hivyo hata wao endapo wataongeza watalipia faini.
Kizuguto alikumbusha timu ambazo zimesajili wachezaji wa kigeni kuwasilisha ada zao ili waweze kupata kbali cha kucheza ligi.
Awali TFF ilitoa muda wa wiki mbili kwa vilabu vyote nchini kukamilisha usajili, ambapo vilabu 13 vya ligi kuu vimeweza kukamilisha ndani ya wakati, klabu 24 vya ligi daraja la kwanza, klabu 24 ligi daraja la pili pia vimeweza kukamilisha usajili wao ndani ya muda uliopangwa.
No comments:
Post a Comment