Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 2, 2015

TAIFA STARS YAONDOKA NA MATUMAINI YA KURUDISHA IMANI KWA MASHABIKI

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa (katikati) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari kuhusu mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi yao na Uganda utaochezwa kesho mjini Kampala. Kulia ni kocha msaidizi, Hemed Morocco na kushoto ni nahodha wa Taifa stars, Nadir Haroub (Picha na Rachel Pallangyo)



WACHEZAJI wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’, Abdi Banda na Mohamed Hussein watakosa mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nakivubo nchini Uganda.

Wachezaji hao ambao ni majeruhi baada ya kuumia kwenye mazoezi hawataweza kusafiri na timu hivyo nafasi zao zimezibwa na wachezaji wengine ambao wapo kambini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kocha Mkuu wa Taifa Stars. Charles Mkwasa alisema kuwa licha ya kuwakosa , Abdi Banda na Mohamed Hussein na Jonas Mkude ambaye alikwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio anaamini wachezaji waliopo watacheza vizuri kwenye mchezo huo wa marudiano wa kutafuta kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)

“Tunashukuru kwa ushirikiano tuliopata toka kwenu waandishi wa habari na mashabiki hivyo tunawaahidi kufanya kile ambacho watanzania wengi wanakitazamia japo tutawakosa wachezaji watatu”, alisema Mkwasa

Pia alisema kipa Mwadini Ally hakuweza kujiunga na kambi ya timu hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia hivyo naye hatosafiri

Taifa stars imeondoka nchini jana jioni kuelekea Kampala - Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The Cranes utakaochezwa Jumamosi  ikiwa na wachezaji 20, bechi la ufundi 7, pamoja na viongozi kwa shirika la ndege la Rwanda (Rwada Airi).

Mchezo wa jumamosi ni wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda, huku mechi hiyo ikichezwa saa 10 jioni katika uwanja wa Nakivubo.

Wachezaji wanaosafiri ni: Ally Mustafa, Mudathir Khamis, Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Michael Aidani, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla, Saimon Msuva, Deus Kaseke, Ramadhan Singano, Atupele Green, Rashid Mandawa, John Bocco na Ame Ally.
Mara baada ya kuteuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mkwasa alitaja kikosi wachezaji 26 na kuwa nacho kambini kwa wiki moja huku wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.

Benchi la Ufundi litaongozwa na Mkwasa, Mshauri wake wa Ufundi, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’, Msaidizi wake Hemed Morocco, kocha wa makipa, Manyika Peter, Mtunza Vifaa Hussein Swedi ‘Gaga’, Meneja Omar Kapilima pamoja na Mratibu Msafiri Mgoyi.
 Stars inatakiwa kushinda 4-0 Jumamosi ili kusonga mbele CHAN

No comments:

Post a Comment