Rais wa shirikisho la soka nchini bolivia Carlos Chavez amekamatwa kama sehemu ya uchunguzi unaohusu ufisadi.
Uchunguzi
huo ulichochewa na hatua za idara ya mahakama nchini Marekani kuhusu
ufisadi ambao umekuwa ukiendelea ndani ya shirikisho la kandanda duniani
FIFA.Bwana Chavez ndiye mueka hazina wa shirikisho la kandanda la nchi za Amerika ya Kusini CONMEBOL
Alikamatwa katika mji wa Sucre nchini Bolivia baada ya kutoa ushahidi kwenye uchunguzi unaohusu ufisadi katika shirikisho la kandanda nchini Bolivia.
Mameneja kadha wa kandanda nchini humo nao wanafanyiwa uchunguzi.
No comments:
Post a Comment