AZAM FC imefuzu kwa asilimia 100 Robo Fainali ya Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kushinda mechi yake
ya tatu na ya mwisho ya Kundi C leo Jumamosi dhidi ya Adama City ya Ethiopia,
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Azam
iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 katika mchezo huo, huku mshambuliaji kutoka
Ivory Coast, Kipre Tchetche akifunga mawili na Farid Mussa, Mudathir Yahya na
Aggrey Morris wakifunga bao moja kila mmoja.
Dakika
45 za kwanza zilimalizika Azam wakiwa mbele kwa mabao 3-0, Kipre akianza dakika
za sita akimalizia krosi ya Ame Ali ‘Zungu’ na dakika ya 18 akimalizia mpira wa
adhabu uliopigwa na Erasto Nyoni.
Nyoni
akamtengenezea Mussa kufunga la tatu dakika ya 31 baada ya kutia krosi maridadi
ya chini chini iliyounganishwa kwa guu la kushoto na kinda huyo aliyekuwa
pembezoni mwa lango la Adama kushoto.
Kipindi
cha kwanza, Adama ilimpoteza mchezaji wake, Eshettu Menna aliyetolewa kwa kadi
nyekundu na mwamuzi Issa Kagabo wa Rwanda baada ya kumkwatua kwa nyuma Mussa
dakika ya 20.
Kipindi
cha pili kilipoanza tu, Yahya akaifungia Azam bao la nne akiunganisha kwa
kichwa krosi maridadi Ame Ali ‘Zungu’ dakika ya 46.
Na
dakika ya 69 Moges Tadese akaoneshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu,
baada ya kuushika kwa makusudi mpira uliopigwa na Yahya na kusababisha penalti
pia.
Kipre
alikosa bao la wazi mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kumpiga tobo kipa
wa Adam City, Yacob Fiseha lakini mpira ukatoka nje sentimita chache.
Beki
mzoefu wa kimataifa wa Tanzania, Aggrey akaenda kuifungia Azam bao la tano kwa
penalti dakika ya 7
Kwa
matokeo haya, Azam inamaliza kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake tisa
ikifuatiwa na KCCA yenye pointi sita ambazo zote zinakwenda Robo Fainali,
wakati Adama imemaliza bila pointi na inarejea nyumbani, huku Malakia ya Sudan
Kusini iliyomaliza na pointi tatu inaweza kufuzu kama mshindi wa tatu
bora.
Kikosi
cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Abdallah Kheri, Serge
Wawa/Said Mourad dk46, Aggrey Morris/Gardiel Miachel, Mudathir Yahya, Hamid
Mao, Jean Baptiste Mugiraneza Ame Ali, Kipre Tchetche/Didier Kavumbangu dk60 na
Farid Mussa.
Adama
City; Yacob Fiseha, Suleman Mohamed, Wendosen Milkesa, Moges Tadese,
Eshetu Menna, Biruk Kelbero, Desalegn Debesh/Wendimeneh
Zerihum dk40, Erkyi Hun Tesfaye, Temesigen Gitsadik/Biniyam Ayele dk46, Takele
Elemayehu na Yonatan Kebede/Henok Gemtesa dk75.
No comments:
Post a Comment