TIMU za
Taifa za soka za wanawake ile ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite na
ile ya wakubwa Twiga Stars, zipo kambini kwa kwa wiki mbili ikiwa ni programu
maalum ya kila mwezi ambayo huandaliwa na Kocha Rogasian Kaijage na kutekelezwa
na TFF.
Timu hizo
zimeweka kambi kwenye hostel za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kufanya
mazoezi kila siku asubuhi na jioni.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu wa timu hizo Kaijage, alisema anafurahi
kuona programu yake inatekelezwa japo si kwa kiwango kikubwa kutokana na timu
hizo kukosa wafadhili.
“Wachezaji
wapo vizuri na wana ari japo tunakosa kambi nzuri kama ilivyo kwa timu za
wanaume kutokana na timu hizi kukosa wafadhili japo TFF wanajitahidi kwa upande
wake hivyo naomba wadau waone haja ya kuisaidia timu hizi za wanawake,”,
alisema Kaijage.
Twiga stars
ina kibarua kigumu cha kupeperusha vema bendera ya Taifa kwenye mashindano ya
wanawake Afrika yatakayofanyika nchini Congo Brazaville, Septemba mwaka huu na
Tanzanite inajiandaa na mchezo wa kutafuta kufuzu fainali za kombe la dunia kwa
vijana wa umri huo dhidi ya Zambia mchezo utakaochezwa Julai mwaka huu.
Timu hizo zimefuzu baada ya kupata matokeo yafuatayo: Nigeria 8-0 Mali (1-1- matokeo ya mechi ya kwanza), Tanzania 2-3 Zambia (4-2), Senegal 1-2 Egypt (0-0), Afrika ya Kusini 5-0 Botswana (0-1), Cameroon 2-1 Ethiopia (2-1) na Zimbabwe 2-2 Ghana (1-2).
No comments:
Post a Comment