MCHEZAJI
Lansana Kamara anayefanya majaribio kwenye klabu ya Yanga, jana aliumia kifundo
cha mguu wa kushoto katika mazoezi ya
asubuhi kwenye uwanja wa Karume.
Kamara
ambaye alianza mazoezi pamoja na wenzake aliumia wakati wa zoezi la upigaji
mashuti marefu hali iliyomfanya alale chali huku akisikilizia maumivu kabla ya
daktari Juma Sufiani kuja kumganga.
Sufiani
alipomfikia alimvua kiatu pamoja na soksi na kumfunga barafu kuzunguka mguu
wote huku akiuwekea sapoti kwa kuuweka juu ya koni ili kupata mlalo mlingano .
Alikaa chini
ya uangalizi wa daktari kwa dakika 30 lakini hata hivyo hakuweza kuendelea na
mazoezi tena.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kocha Mkuu wa Yanga Hans van Der Pluijm,
alisema anashukuru mazoezi yake yanaendelea vizuri na kusema anaweza
kumzungumzia Kamara baada ya kucheza mchezo wa kirafiki.
“Natarajia
Juni 26 au 27 nitakuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Vital O ya
Burundi baada ya kucheza michezo miwili ndo naweza kumzungumzia Lansana,”
alisema Pluijm.
Kamara
ambaye ni raia wa Sierra Leone ni wiki moja imepita tangu ajiunge kwenye mazoezi ya Yanga
akifanya majaribio na kikosi hicho
kusaka nafasi ya kusajiliwa msimu ujao.
No comments:
Post a Comment