SHIRIKISHO
la Soka Tanzania(TFF) limetangaza kujiunga na Asasi ya GSI kwa ajili ya kuweka barcode
(msimbomilla) au alama hiyo kwenye jezi za timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ili kuwa
rahisi kudhibiti mapato na uuzaji holela wa bidhaa hizo.
GSI ni
Shirika la Kimataifa linalojihusisha na udhibiti wa bidhaa zinazozalishwa,
ambapo Tanzania ni mwanachama kwa namba 620 tangu mwaka 2011 wakifanya kazi na
zaidi ya makampuni 780 .
Akizungumza leo na waandishi wa habari Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema wamejiunga na GSI
ili kupata alama hiyo itakayowasaidia kudhibitiza wizi lakini pia, uuzwaji
holela wa jezi hizo.
“Tunaamini alama
ya GSI ikiwapo katika jezi tutakomesha watu ambao wamekuwa wakiuza jezi feki,
na wale wote wenye makontena Kariakoo, wajue kuwa sasa tutauza zile zenye alama
hii, tupate mapato yetu kwa manufaa ya Shirikisho,”alisema.
Alisema hata
klabu kama zinahitaji kudhibiti mapato yao, ni muhimu zikajiunga huko kuwekewa
nembo hiyo kwenye jezi.
Naye Ofisa
Mtendaji Mkuu wa GSI, Fatma Kange alisema jezi ikiwa na alama (barcode) itauzwa
popote katika maduka mbalimbali makubwa kwa vile itakuwa na nembo inayojulikana
kimataifa.
Alisema watafurahi
pia, ikiwa watapewa nafasi katika kuweka alama hizo kwenye tiketi za kuingilia
uwanjani, kwani kazi yao ni kubwa huku akisema hata vyuo vikitaka kujua ni kwa
jinsi gani watapambana na wanafunzi wasiolipa ada wanasuluhisho.
No comments:
Post a Comment