RAIS wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amesema Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Mart
Nooij akishindwa kuivusha timu katika michuano ya Afrika kwa wachezaji wa
ndani (CHAN) kibarua chake kitaota mbawa.
Kauli hiyo
imekuja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kpcha huyo kunyooshewa vidole na wadau
wa soka kwa kushindwa kufanya vizuri kuanzia kwenye michuano ya Baraza la Vyama
vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA) na mchezo dhidi ya Misri kufuzu michuano ya
Afrika uliochezwa juzi.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari leo Malinzi alisema Nooij alipewa muda wa
kuhakikisha anaivusha Taifa Stars katika michuano ya CHAN, na kwamba baada ya
kurejea atajiandaa kwenda Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa CHAN wa kwanza dhidi ya Uganda.
“Kamati ya
Utendaji ya TFF ilimpa Kocha jukumu la kuivusha Tanzania katika michuano ya
CHAN, tunataka kushiriki michuano hii itakayofanyika nchini Rwanda,” alisema.
Baada ya
mchezo huo wa Jumamosi, mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda utachezwa Julai 4,
mwaka huu nchini Uganda.
Baadhi ya
wadau wa soka wamekuwa wakipendekeza kufukuzwa kwa Kocha huyo wakidai kuwa
ameshindwa kusaidia timu hiyo.
Miongoni mwa
wadau hao ni Rais wa zamani wa Simba Ismail Rage, ambaye ameonyesha kukerwa na
matokeo mabovu ambayo Taifa Stars imekuwa ikiyapata na kupendekeza umuhimu wa
kutimuliwa kwa Kocha huyo.
No comments:
Post a Comment