Timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium
Lager, imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizi ya mchezo
wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania kufuzu kwa CHAN 2016.
Msafara wa
Taifa Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao wamefikia
katika hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhid ya Uganda utachezwa katika uwanja wa
Amani kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia majira ya saa 2 usiku.
Stars inakutana
na Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa
Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda,
kabla ya kurudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.
Mara baada
ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea na kambi katika
hoteli ya Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa Karume kabla ya kuondoka
leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar.
Kocha mkuu
wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao hawakua katika
kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania
kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN wikiendi hii.
Wachezaji
waliongezwa ni Atupele Green, Hassan Isihaka, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa na
Kelvin Friday, wanaungana na wachezaji Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomary
Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris na Nadir Haroub.
Wengine ni
Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi Haji, Abdi Banda, Frank Domayo, Amri Kiemba,
Said Ndemla, Saimon Msuva, na John Bocco.
Aidha, Shirikisho la Soka Tanzania (CAF), limetoa mwongozo kuwa
mchezaji Mrisho Halfan Ngasa haruhusiwi kucheza CHAN kwa sababu sio mchezaji
tena wa ndani, hivyo Ngasa ameondolewa kikosini
Waaamuzi
wa mchezo huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao ni Hudu Munyemana
(Rwanda), akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda), Justin Karangwa (Rwanda),
mwamuzi wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na kamishina wa mchezo Nicholaus
Musonye kutoka Kenya.
No comments:
Post a Comment