Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, June 16, 2015

ROBERTO FIRMINO NJIA NYEUPE KUJIUNGA NA UNITED

Wakala wa Fowadi wa Hoffenheim Roberto Firmino amethibitisha kuwa Mchezaji huyo anahamia England kwa ajili ya Msimu ujao.

Roger Wittmann, ambae anamwakilisha Nyota huyo mpya anaewika kutoka Brazil mwenye Miaka 23, amekataa kutoboa waziwazi ni Klabu ipi Mchezaji wake huyo atakwenda ingawa hivi karibuni amehusishwa na kujiunga na Manchester United.
Akiongea na Gazeti la Ujerumani, Bild, Wittmann amesema: "Ninachoweza kusema ni kuwa anahamia England!"
Hivi sasa Firmino yuko huko Nchini Chile akiwa na Timu ya Taifa ya Brazil inayocheza Fainali za Copa America, Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini.
Firmino, ambae aliifungia Hoffenheim Bao 7 kwenye Bundesliga Msimu uliopita, anathaminiwa kati ya Pauni Milioni 18 na 21.7 na ikiwa atauzwa kwa Dau hilo basi ataweka Rekodi ya kuuzwa kwa Bei kubwa toka Klabu hiyo ya Germany kwani Rekodi yao ni pale walipomuuza Carlos Eduardo kwenda Rubin Kazan kwa Pauni Milioni 14.5.

No comments:

Post a Comment