Liverpool
imekataa ombi la kitita cha pauni milioni 25 na nyongeza ya pauni
milioni 5 kutoka kwa Manchester City ili kumnunua Raheem Sterling.
Pia
inaaminika kwamba Liverpool inamthamini mchezaji huyo wa miaka 20 kuwa
na thamani ya pauni milioni 50 na kwamba haina mpango wa kumuuza .
Hatahivyo ajenti wa Sterling Aidy Ward amedaiwa kusema kwamba hatokubali kandarasi nyengine katika klabu ya Liverpool hata akipewa kandarasi ya pauni laki tisa kwa wiki.
No comments:
Post a Comment