SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemzuia kiungo
mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa kuicheze timu ya
taifa, Taifa Stars dhidi ya Uganda kesho
CAF imeiambia TFF kwamba Ngassa haruhusiwi tena kucheza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), kwa sababu siyo mchezaji wa Ligi ya ndani.
Ngassa aliyesaini Mkataba wa miaka minne na Free State Stars ya Afrika Kusini Mei mwaka huu akitokea Yanga SC ya Tanzania kwa sababu hiyo ameondolewa kwenye kikoso kitakachoivaa Uganda.

Taifa Stars imeshafika Zanzibar
ikiwa na wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao wamefikia katika hoteli ya
Nungwi Inn.
Stars inakutana na Uganda katika
mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa
wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda, kabla ya
kurudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN wikiendi hii.
Wachezaji waliongezwa ni Atupele Green, Hassan Isihaka, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa na Kelvin Friday, wanaungana na wachezaji Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris na Nadir Haroub.
Wengine ni Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi Haji, Abdi Banda, Frank Domayo, Amri Kiemba, Said Ndemla, Saimon Msuva, na John Bocco.
Waaamuzi wa mchezo huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao ni Hudu Munyemana (Rwanda), akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda), Justin Karangwa (Rwanda), mwamuzi wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na kamishina wa mchezo Nicholaus Musonye kutoka Kenya.

No comments:
Post a Comment