Baadhi ya maamuzi yake ni haya yafuatayo:
- TUNZO ZA VODACOM.
Baada
ya kuzingatia mapungufu yaliyojitokeza katika uteuzi wa tuzo za ligi
kuu ya Vodacom msimu wa 2014/15, Kamati ya utendaji imeagiza Rais wa TFF
aunde kamati maalum ya kusimamia mchakato wa utoaji wa tuzo za Vodacom.
Kamati hii itazingatia umuhimu wa kuhusisha idara za ufundi za TFF
katika zoezi hilo na wadhamini na ligi watahusishwa kwa ukaribu katika
zoezi hili.
- KANUNI ZA LIGI 2015/16.
Kamati ya utendaji ilipitia rasimu ya kanuni za ligi kuu, FDL na SDL za msimu ujao wa 2015/16.
Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kwenye maeneo yafuatayo:
- LESENI ZA VILABU.
Kamati
ya utendaji imesisitiza kuwa hakuna klabu itakayopitishiwa usajili wake
kama kupewa leseni ya klabu ya msimu.( Club Licencing).
- WAAMUZI.
Kamati
ya utendaji imeridhia wazo la kamati ya maamuzi kuwa kuanzia msimu
2015/16 kutakuwa na jopo maalum ya waamuzi ( Elite referees)
litakalochezeshwa mechi zote za ligi kuu.
Waamuzi hawa watakuwa ni 16 wa kati, 32 wa pembeni na 4 wa akiba. Hii itasaidia kuongoza ufanisi katika uamuzi. (refereeing).
- MGAWANYO WA MAPATO YA MILANGONI.
Vilabu
vimeongezwa mgawanyo wa mapato ya milangoni na sasa vitakuwa
vinachukua asilimia 60% ya mapato ya mlangoni, makato mengine ni 18% VAT
na 15% gharama za uwanja.
- UDHIBITI WA WACHEZAJI.
Kanuni ilikuwa inatoa fursa timu ya kuamua mechi ipi mchezaji asicheze baada ya kuwa na kadi tatu za njano imefutwa.
- KUSAJILI MIKATABA YA WACHEZAJI.
Kuanzia
sasa mikataba kati ya wachezaji na klabu itakayotambuliwa na TFF
itakuwa ni ile ambayo ni nakala halisi zilizopigwa muhuri na lakiri ya
TFF na kusajiliwa kwenye kumbukumbu ya TFF. Vilabu na mwachezaji
watapewa nakala hizi baada ya kusajiliwa na TFF.
- WACHEZAJI WA KIGENI.
Kamati
ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu 2015/16 idadi ya wachezaji wa
kigeni watakaosajiliwa na klabu ya ligi kuu itakuwa 7 (saba) wachezaji
wote hawa, wote wataruhusiwa kucheza kwa wakati wote.
Mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo:
- Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za Taifa za nchi yake ( Senior, U23, U20, U19, U17 nk) au
- Mchezaji awe anacheza katika ligi kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.
- Kila mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa vijana ya dola 2,000 kwa kila msimu atakyocheza hapa nchini. Fedha hizi zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira (Football Development Fund).
Pia
imeamriwa kuwa mikataba ya vilabu na wachezaji iliyo hai itaendelea
kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini wataruhusiwa
kuuhisha (to renew) mikataba yao iwapo watakubaliana na vilabu vyao.
4. LESENI ZA MAKOCHA
Kamati
ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu huu, Kocha wa timu ya ligi kuu
sharti awe na leseni B ya CAF au itakayolingana nayo kutoka katika
mashirikisho mengine duniani na kocha msaidizi awe na leseni C ya CAF,
hii ni kwa misimu mitatu.
Kuanzia
msimu wa 2018/2019 kocha wa Ligi Kuu atatakiwa kuwa na leseni A ya CAF
au inayolingana na hiyo kutoka katika mashirikisho mengine duniani.
Aidha
Kamati ya Utendajji ya TFF imemteua Meshack Bandawe kuwa mjumbe wa bodi
ya mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu - TFF (FDF), Bandawe ni meneja
wa PPF kanda ya ziwa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment