Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza Dylan Kerr kwa kocha wa makipa Idd Salim (kulia) baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. |
KOCHA mpya
wa Simba, Muingereza Dylan Kerr amesema ataendeleza wachezaji chipukizi ili kuwa
na timu bora kwa sasa na baadae.
Kerr
aliyasema hayo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere na kulakiwa na wajumbe wa Kamati ya Simba, Collin Frisch na Said Tully.
“Nimefurahi
kuja Tanzania na nawaahidi viongozi na mashabiki kuwa nitahakikisha naendeleza
wachezaji chipukizi hili Simba iweze kutamba sasa na baadae”, alisema Kerr.
Kocha huyo
ambaye amerithi mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha
Simba ambapo atakuwa anasaidiwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo Suleman
Matola.
Wakati Kerr
akiwasili pia alikutana na kocha mpya wa makipa Idd Salim toka Kenya ambaye
naye aliwasili tayari kwa kazi yake mpya kwenye klabu ya Simba.
Simba
waliamua kuachana na Kopunovic na kusaka kocha huyo mpya baada ya Mserbia huyo
kuhitaji Simba imlipe kiasi cha Dola za Marekani 50,000 (sh. Milioni 100) kama
ada ya usajili na mshahara wake ambapo kila mwezi atakuwa analipwa dola za
Marekani 14,000 9sh. Milioni 28).
Baada ya
kushindwana kwenye malipo ndipo uongozi uliamua kumsaka kocha mpya na kumpata
Kerr ambaye inasemekana atalipwa mshahara wa dola za marekani 9,000 sawa na
milioni 18 kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment