UONGOZI wa Coastal Union,Wagosi wa
Kaya umeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar,
Jackson Mayanja kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao
wa Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu .
Kocha huyo ambaye ni raia wa Uganda,
ameingia karandasi ya kuinoa Coastal Union leo jijini Tanga mbele ya Katibu
Mkuu wa timu hiyo, Kassim El Siagi na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter.
Akizungumza kwa njia ya simu baada
ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wana imani ataipa mafanikio
timu yao katika ligi kuu msimu ujao.
“Uwezo wa kocha Mayanja unatupa matumaini
makubwa ya mafanikio ukizingatia ana
uwezo wa kufundisha na kupata mafanikio hivyo tunaamini kuja kwake kwetu
itakuwa chachu katika maendeleo”, alisema Assenga
Mayanja aliwahi kuzifundisha timu za
soka Kiyuvu FC ya Rwanda,timu ya Mamlaka ya Mapato (URA),Vipers FC ya
Bunamwaya na KCC zote za Uganda amesema kutua kwake kwenye timu Coastal
Union kunampa faraja hivyo atahakikisha anatoa mchango wake kuipa mafanikio.
Pia alisema mipango yake ni
kuhakikisha timu inang’ara katika michuano ya ligi kuu msimu ujao ikiwa ni
pamoja na kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuhirikiana
na wachezaji, mashabiki na uongozi kwenye medani za kitaifa na kimataifa.
No comments:
Post a Comment