Mchezaji wa Yanga Juma Abdul (kulia0 akimtoka mchezaji wa Friends Rangers leo kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume |
TIMU ya
Yanga yenye maskani yake mtaa wa Jangwani na Twiga jana iliifunga Friends
Rangers mabao 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume jijini
Dar es Salaam.
Yanga ambayo
ilikuwa inawajaribu wachezaji wake ambao wamesajiliwa msimu huu ilianza kupata
bao la kwanza dakika ya 11 lililofungwa na Kpah Sherman akimalizia pasi ya
Busungu
Hata hivyo
Friends Rangers walisawazisha bao hilo dakika ya 25 lililofungwa na Mussa Juma lakini
dakika ya 37 Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na Busungu baada ya
kupokea pasi toka kwa Sherman bao lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha
pili kila timu ilifanya mabadilikoambapo Yanga iliwatoa Kpah Sherman, Geofrey Mwashaiya,
Andre Countinho na kipa Benedicto Tinoco na kuwaingiza kipa Ally Mustapha ‘Barthez’,
Amis Tambwe, Simon Msuva na Deus Kaseke.
Mabadiliko
hayo yaliongeza mashambulizi kwani kila mchezaji alijitahidi kuwafurahisha
mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo lakini mchezaji Cosmas Lewis wa Friends
Rangers aliwanyamazisha mashabiki baada ya kusawazisha bao dakika ya 83 kabla
ya Busungu kuifungia Yanga bao la ushindi dakika ya 88.
Friends
Rangers ambao wanacheza ligi daraja la kwanza tena bado hawajaanza mazoezi walionyesha
kandanda safi mbele ya Yanga ambayo imeanza mazoezi takribani wiki mbili sasa
huku ikiwa na wachezaji wake wa kigeni.
No comments:
Post a Comment