MSHAMBULIAJI
wa timu ya Stand
United,Abasarim Chidiebele akizungumza na waandishi wa habari mkoani
Tanga mara baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu ya
Coastal Union, Picha na Mwandishi Wetu,Tanga
MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United,
Abasarim Chidiebele, amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya Coastal
Union kwa mkataba wa mwaka mmoja katika msimu ujao wa Ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara. Chidiebele alitua mkoani Tanga juzi kwa ajili
ya kuingia makubaliana na uongozi wa timu ya Coastal Union ambapo
utiliaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa
Coastal Union, Kassim El Siagi, Meneja wa Coastal Union, Akida Machai
na viongozi wengine. Akizungumza mara baada ya kusaini, Chidiebele
amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na Coastal Union na kuhaidi kutumia
uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo katika
michuano ya Ligi kuu msimu ujao. “Nashukuru kusajili
Coastal Union kikubwa niwahidi tu wapenzi, wanachama na mashabiki
kutumia uwezo wangu katika kuipa mafanikio timu yetu" Alisema
Mshambuliaji huyo ambaye ni tishio hapa nchini. Kwa upande wake,
Ofisa Habari wa Klabu ya Coastal Union, Oscar Assenga alisema kuwa msimu
huu timu hiyo imedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakaowawezesha
kuhakikisha wanachukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara. “Unajua
usajili wetu sio wa kukurupuka hivyo lazima tuwe makini kwani hiyo ndio
itakuwa njia pekee ya kuhakikisha tunatimiza mipango yetu ya kuchukua
Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao “Alisema. Hata hivyo aliwataka
wapenzi mashabiki kuweka mshikamano wa pamoja ambao utatuwezesha
kufanikisha malengo yao ya mwakani kushiriki kombe la shirikisho kwa
kuanza kufanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu. Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment