Mshambulizi
wa Togo Emmanuel Adebayor atacheza dhidi ya Liberia hapo leo katika
mechi ya mkondo wa kwanza ya kuwania nafasi ya kushiriki kombe la
mabingwa barani Afrika.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 ameratibiwa kushambulia Liberia licha ya kuwasili kambini akiwa amechelewa.Adebayor ambaye hakushiriki mechi ya kupimana nguvu baina ya Togo na Black Stars ya Ghana amekuwa na wakati mgumu kikosini baada ya kocha
Tom Saintfiet kumkashifu mshambulizi huyo wa klabu ya Uingereza ya Tottenham Hostpurs kwa kuwa mtundu.
Adebayor ameiambia dawati la michezo la BBC kuwa alichukua fursa ya kumweleza kocha Saintfiet
kuwa mechi hiyo haikuwa na umuhimu wowote kwao na hivyo alikuwa radhi asiicheze .
Hata hivyo mshambuliaji huyo alisema kuwa ''Tofauti na mechi ya Ghana ,mechi hii ya hapo kesho dhidi ya Liberia inaumuhimu mkubwa sana kwetu.
Iwapo tunataka kufuzu kwa mkondo ujao wa kuwania nafasi ya kombe la mabingwa barani Afrika, hatuna budi ilakuishinda.''
Kocha Saintfiet amethibitisha kuwa Adebayor - Kossi Agassa na Floyd Ayite - watakuwa uwanjani katika mechi hiyo muhimu.
No comments:
Post a Comment