KAMATI ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imepunguza
idadi ya waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu na kuwaongezea posho. Imeelezwa kuwa
idadi ya waamuzi itapunguzwa kutoka 90 msimu
uliopita hadi kufikia 48 msimu ujao.
Aidha,
posho ya waamuzi hao itaongezwa mara mbili ya mwaka jana, kutoka Sh 250,000
hadi 500,000. Akijibu maswali ya waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Salum Chama alisema kati ya hao, waamuzi wa kati watapunguzwa kutoka 26
walioteuliwa mwaka jana, hadi kubaki 16 wakati wasaidizi watapungua kutoka 64
msimu uliopita hadi 32.
“Tumeona
tupunguze idadi kupunguza changamoto, ambazo zimekuwa zikilalamikiwa lakini pia
tunataka ligi yetu ichezeshwe kwa ubora wa hali ya juu,” alisema.
Chama
alisema vigezo walivyotumia katika kupunguza idadi hiyo vimetokana na ripoti ya
msimu uliopita, mechi walizochezesha, uwezo
na umri usiozidi miaka 45.
Alisema
wanategemea baada ya kupunguza idadi hiyo ligi itachezeshwa kwa kuzingatia
sheria 17 za soka na itakuwa bora zaidi na hakutakuwa na malalamiko yasio ya
lazima.
Alisema
nia yao ni kuhakikisha ligi inakuwa na ubora ukilinganisha na miaka iliyopita,
pia kuondoa vishawishi dhidi yao.
Kuhusu
posho alisema wameona waboreshe kiwango ili kutoa nafasi kwa waamuzi kuepuka vishawishi
vya kupokea rushwa.
Inaendelea Uk. 31
No comments:
Post a Comment