Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa
Bodi ya Ligi Kuu nchini.
Uteuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha kamati
ya Utendaji ambapo awali kabla ya uteuzi huo atakaoanza kuutumikia rasmi Juni 1
mwaka huu alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.Pia aliwahi kuitumikia TFF kama
Afisa Habari wake.
Pia Kamati hiyo ya utendaji imemteau Martin
Chacha ambae ni mratibu wa timu za Taifa kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashindano
TFF iliyoachwa na Wambura.
Pia kikao hicho kilifanya mabadiliko na
kumteua Leopald Tasso Mkebezi kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.
Mkebezi aliwahi kuwa meneja wa timu hiyo ya
Taifa katika kipindi cha miaka sita kuanzia 2006 - 2012.
Pia wajumbe sita waliteuliwa kuongoza Mfuko wa FDF ambao ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya mkutano
mkuu wa TFF ulioingiza kipengele cha FDF katika katiba yake.
Mfuko huo utaongozwa Mwenyekiti wake Tido
Mhando, ambapo Makamu wake ni Deogratius Lyatto.
Wajumbe ni pamoja na Ephraim Mafuru, Beatrice
Singano, Joseph Kahama pamoja na Ayoub Chamshana huku Henry Tandau akiwa ndio katibu
mtendaji wa mfuko huo.
No comments:
Post a Comment