Kocha
Mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij, amewaita wachezaji 16 kuingia kambini
kesho siku ya jumatano kwa ajili ya kupimwa afya zao na kujua maandeleo
yao kabla ya kuwajumisha katika kikosi cha pamoja kitakachokua kwenye
maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.
Wachezaji
walioitwa kuingia kambini kesho ni, Mohamed Hussein, Peter Manyika,
Hassan Isihaka, Jonas Mkude (Simba SC), Salum Telela, Juma Abdul, Nadir
Haroub (Yanga SC), Aishi Manula, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Kelvin
Friday (Azam FC), Rashid Mandawa, Atupele Green (Kagera Sugar), Haroun
Chanongo (Stand United) Malimi Busungu (Mgambo JKT) na Emmanuel Simwanda
(African Lyon).
Mara
baada ya kurejea kutoka nchini Afrika Kusini, kocha wa Stars Nooij
aliwapa mapumziko ya siku 10, wachezaji waliokua kwenye michuano ya
Cosafa mpaka Juni Mosi ambapo ndipo watajumuika na wachezaji wengine
waliopo kambini.
Ifikapo
Juni Mosi, 2015 Taifa Stars itaanza kambi ya moja kwa moja kujiandaa na
mechi dhidi ya Misri itakayochezwa jijini Alexandria katika uwanja wa
Borg El Arab Juni 14, 2015 ikiwajumuisha pia wachezaji Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe
ya Congo DR.
Kabla
ya kuelekea nchini Misri, Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi jijini
Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia tarehe 4,Juni 2015 kwa muda wa wiki
moja kabla ya kuelekea nchini Misri kwenye mchezo huo dhidi ya Mafarao.
Juni
20, 2015 Taifa Stars itawakaribisha Uganda kwenye uwanja wa Aman mjini
Zanzibar katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa
wachezaji wa ndani CHAN, zitakazofanyika nchini Rwanda 2016, na mchezo
wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili nchini Uganda.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment