Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 6, 2015

BONDIA CHEKA KUPANDA ULINGONI MEI 30 P.T.A SABASABA


 


BONDIA Francis Cheka anatarajia kupanda ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela Mei 30 kupambana na bondia Kiatchai Singwancha kutokaThailand.

Pambano hilo litakuwa la raundi kumi na utachezwa kwenye Ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia pambano hilo promota Kaike Siraju amesema kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa na mabondia wa utangulizi wote wanatarajia kusainishwa mkataba wa kupanda ulingoni wiki hii.
“Tumeandaa pambano hili kwa ajili ya kumkarisha ndugu yetu Cheka ambaye anatumikia kifungo cha nje baada kupatikana na hatia ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kumpiga meneja wa baa”, alisema Siraju
Pambano litasimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini P.S.T chini ya rais wake Emanuel Mlundwa
Siraju amesema kuwa bondia wa Thailand atawasili nchini siku tatu kabla ya pambano hivyo kuwatakamashabiki kwenda kumwona kipenzi chao Cheka akiwa furaha baada ya kimya kirefu

No comments:

Post a Comment