
Bao la ushindi la Azam FC lilifungwa Dakika ya 24 na Straika kutoka Burundi Didier Kavumbagu na hilo ni Bao lake ka 10 Msimu huu kwenye Ligi.
Ushindi huu umewapa uongozi Azam FC sasa wakiwa na Pointi 33 kwa Mechi 17 wakifuata Yanga wenye Pointi 31 kwa Mechi 16 na Simba wako Nafasi ya 3 wakiwa wamecheza Mechi 18 na wana Pointi 29.
Mbali ya kuwa kileleni ushindi huu umewapa raha Azam FC ya kulipa kisasi cha kufungwa 1-0 na Ndanda FC huko Nangwanda Mtwara katika Mechi ya kwanza.
No comments:
Post a Comment