SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema litashirikiana na Wakala wa
Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuhakiki umri wa wachezaji watakaoshiriki mashindano ya Copa Cocacola yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuhakiki umri wa wachezaji watakaoshiriki mashindano ya Copa Cocacola yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Hatua
hiyo imefikiwa ili kukwepa mikoa kudanganya umri kwa wachezaji kwani mwaka huu
mashindano yatahusisha wachezaji waliochini ya miaka 15.
Akizungumza
jijini leo, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho hilo, Boniface Wambura,
alisema kuwa wachezaji watakaobainika kuzidi umri hawataruhusiwa kushiriki
katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 15.
Pia alisema kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya
michuano kuhusu idadi ya wachezaji, kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji
wasiozidi 20 na wasiopungua 16 hivyo kila timu inatakiwa kuhakikisha inakuwa na
idadi hiyo ya wachezaji, kwani kikanuni wakipungua 16 itaondolewa kwenye
mashindano.
Wambura ameitaka mikoa ya Arusha, Dodoma,
Katavi, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Mjini Magharibi na Simiyu kuwasilisha
usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola
2014 kabla ya Desemba 5 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya
michuano hiyo, mkoa ambao hautawasilisha usajili wake kwa ajili ya uhakiki wa
umri wa wachezaji utakaonza Desemba 10 mwaka huu utaondolewa katika fainali
hizo ambazo zitamalizika Desemba 20 mwaka huu.
Timu 16 kwa upande wa wavulana zitashiriki
katika fainali hizo wakati kwa upande wa wasichana ni timu nane. Mikoa
iliyoingiza timu za wasichana kwenye fainali hizo ni Arusha, Dodoma, Ilala,
Kinondoni, Mbeya, Mwanza, Temeke na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment