MWAMUZI wa aliyechezesha mechi ya mtani jembe, Jonesia Rukyaa amepata
beji ya FIFA na waamuzi wengine wa kike sita.
Jonesia ambaye alimudu vema kuchezesha mchezo huo uliochezwa Uwanja wa
Taifa Desemba 13, mwaka huu na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Yanga amepata beji hiyo na Florentina Zablon toka Dodoma na Sophia Ismail toka
Mara kama waamuzi wa kati huku waamuzi wasaidizi wakiwa ni Hellen Mduma wa Dar
es Salaam, Kudra Omary toka Tanga, Grace Wamala toka Kagera na Dalila Jaffary
toka Zanzibar.
Katika taarifa ambayo imeweka kwenye blogu http://refereesfifa.blogspot.com
inasema kuwa Israel Mujuni wa Dar es Salaam, Waziri Sheha wa Zanzibar, Martin
Saanya wa Morogoro na Mfaume Nassoro wa Zanzibar wamepata beji hizo kama
waamuzi wa kati huku Samwel Mpenzu wa Arusha, John Kanyenye wa Mbeya, Frednand
Chacha wa Mwanza, Josephat Bulali wa Dar es Salaam, Sudi Lila na Frank Komba wa
Pwani wakipata beji hizo kama waamuzi wasaidizi.
Tanzania imepata beji nyingi za FIFA kwa upande wanawake msimu huu wa
2015 kwani haijawahi kupata beji zaidi ya nne kuanzia ianze kutoa waamuzi wa
kike kwani hata mwaka huu haikuwa na mwamuzi mwenye beji wa kike.
Waamuzi wa kike ambao walishawahi kuwa na beji za FIFA ni kuanzia 2006
ni Flora Kashaija, Isabela Kapera na Judy Gamba kama waamuzi wa kati na waamuzi
wasaidizi ni Zahara Mohamed, Saada Tibabimale, Mwahija Omary toka Zanzibar.
Katika historia ya soka la Tanzania huwezi kuacha kumtaja Elizabeth
Kalinga toka Mbeya lakini hakubahatika kupata beji ya FIFA kwani umri wake
ulikuwa umepita wakati FIFA ilipoanza kutoa beji hizo kwa Tanzania
No comments:
Post a Comment