KIPA Juma
Mpongo anachezea Seeb ya Muscat, Oman leo analazimika kukosa mchezo kombe la sultan dhidi ya timu ya Oman club
baada ya kuumia akiwa mchezoni hali iliyosababisha kuzimia zaidi ya dakika 30
wiki iliyopita.
Mpongo aliumia wakati timu yake ikicheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Boshar
na kukimbizwa hospitali ya Badri Alsamaa and Polyclinic,
mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bila
kufungana
Akizungumza
kwa njia ya mtandao wa kijamii, Mpongo alisema aliumia wakati akiruka kupangua
krosi iliyopigwa na wachezaji wa timu pinzani hali iliyosababisha kugongana
ndipo akapoteza fahamu na alikuja kuzinduka akiwa hospitali.
“Nilikuwa
naruka kuokoa krosi ya wapinzani wetu ndipo tulipogongana na na kilichoendelea
sikijui kwani nilipokuja kupata fahamu nilijikuta nimelazwa hospitali”, alisema
Mpongo.
Kipa huyo
aliyewahi kudakia Yanga, Coastal Union ya Tanga na Ashanti United ya Ilala amesema
kabla ya juzi, wiki moja iliyopita aliumia tena kwenye ini wakati wakicheza na
Boshar kwenye michuano ya Kombe la Mazda lakini alipofanyiwa vipimo kwa zaidi
ya saa nne ilionekana ini halijaumia.
Mpongo
anasema ni mara ya kwanza kuzimia akiwa mchezo pia anatarajia kuanza mazoezi
madogomadogo kesho pia anawaasa magolikipa wenzake kuwa makini wakati wakicheza
mipira ya krosi kwani washambuliaji wajanja hutumia nafasi hiyo kujaribu
kuwaumiza.
No comments:
Post a Comment