WAKATI
Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney Leo hii akipimwa Goti lake
kuthibitisha undani wa maumivu yake na pia atakuwa nje kwa muda gani,
Klabu hiyo imepata habari njema baada ya Kiungo Daley Blind kupata nafuu
na huenda akawa fiti kabisa kabla ya mwisho wa Mwezi huu baada nae
kuumia Goti.
Rooney hakucheza Mechi ya Ligi Kuu England Jumanne Usiku Uwanjani Old Trafford wakati Man United inaifunga Stoke City 2-1 baada kuumia Goti Jumamosi iliyopita wakati wanaifunga Hull City.
Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema: “Rooney atachunguzwa zaidi Goti lake Jumatano. Natumai hakuumia sana.”
Nae Blind alieumia Goti akiichezea Timu ya Taifa ya Netherlands anatarajiwa hivi karibuni kurejea Mazoezini.
Tangu aanze kuifundisha Man United, Van Gaal amekumbwa na Majeruhi wengi na kwenye Mechi na Stoke City Mastaa wake wakubwa kina Angel Di Maria, Luke Shaw na Daley Blind vile vile hawakucheza.
Van Gaal amethibitisha kuwa Rooney na Di Maria hawataweza kucheza Mechi yao ijayo ya Ligi Jumatatu Ugenini na Southampton kwani ni mapema mno kwao.
Hata hivyo, Van Gaal amesema majeruhi wao wengi sasa wanapona na wameanza kurejea Mazoezini.

No comments:
Post a Comment