WINGA wa Manchester United Angel Di Maria ndie ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Nchi yao Argentina kwa Mwaka huu 2014.
Angel Di Maria amevunja himaya ya Lionel Messi kuitwaa Tuzo hiyo mfululizo tangu Juan Sebastian Veron, Mchezaji mwingine aliewahi kuichezea Man United, kuitwaa Mwaka 2006.
Tangu 2007 Messi ameitwaa Tuzo hiyo bila upinzani lakini Msimu huu Angel Di Maria ndie alieipa Real Madrid Decima yaani kutwaa Kombe la Ulaya mara 10 na pia ndie aliefunga Bao la ushindi Dakika za Nyongeza dhidi ya Switzerland na kiwezesha Argentina kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Julai.Lionel Messi aliyekuwa kinganganizi wa hii tuzo kwa muda mrefu.
Di Maria (kushoto) Van Persie na Mata walipomtembelea mtoto aliyekuwa anaumwa Hospitali hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment