Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 14, 2014

WAYNE ROONEY: SITAKUWA LEJENDARI ENGLAND KAMA SIR BOBBY CHARLTON BILA KOMBE LA DUNIA

NAHODHA wa England Wayne Rooney ameungama hawezi kuwa Lejendari wa England kama Sir Bobby Charlton bila ya kutwaa Kombe la Dunia.Wayne Rooney during training
Rooney, Nahodha wa Manchester United mwenye umri wa Miaka 29, anahitaji Bao 7 zaidi kuifungia England ili ampiku Sir Bobby Charlton ili awe Mfungaji Bora katika Historia ya England.
Wayne Rooney during training
Mbali ya Sir Bobby Charlton kuishikilia Rekodi hiyo ya England ambayo alistaafu kuichezea Mwaka 1970, pia aliisaidia England kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 1966 lilipochezwa Nchini Uingereza.
Hivi sasa Sir Bobby Charlton ni mmoja wa Wakurugenzi wa Manchester United.
Jack Wilshere, Theo Walcott and Wayne Rooney
Akiandika kwenye Makala maalum ya Programu ya Mechi ya Kundi E la EURO 2016 ambapo England Jumamosi watacheza na Slovenia na Rooney kufikisha Mechi 100 kwa Nchi yake, Rooney alisema: “Ni wazi sitakuwa Lejendari mkubwa kama Sir Bobby Charlton kwa sababu yeye ametwaa Kombe la Dunia! Ili kumpiku inabidi nishinde Kombe la Dunia!”
England manager Roy Hodgson gives instructions to his players
Akiongelea Rekodi ya Ufungaji Mabao kwa England, Rooney alisema: “Rekodi hii imesimama kwa muda mrefu na wapo Wachezaji wengi wameshindwa kuivunja! Mie bado kijana na naamini naweza kuivunja!”Roy Hodgson gestures during a training session
Jumamosi huko Wembley, Rooney, ambae ni Nahodha wa England, ataiongoza Timu kuingia Uwanjani akiambatana na Watoto wake wawili wa Kiume, Kai na Klay, na kisha kukabidhiwa Kofia ya Dhahabu na Sir Bobby Charlton ikiwa ni Tuzo maalum kwa kuichezea England Mechi 100. 
England players observe a two-minute silence on Armistice Day during a training session at St George's Park
Mapema Meneja wa England, Roy Hodgson, ambae ndie alimteua Rooney kama Nahodha, alimsifia Mchezaji huyo kwa ushujaa wake na kueleza: “Alivamia Soka na kuibuka kama Kijana wa ajabu mwenye kipaji. Alikuwa mkombozi wa Soka la England. Baadae akawa anasulubiwa akishindwa kuiokoa England na Watu wamemponda kwa hilo!”

Wafungaji Bora:ENGLAND 
-Sir Bobby Charlton: Goli 49 Mechi 106
-Gary Lineker: Goli 48 Mechi 80
-Jimmy Greaves: Goli 44 Mechi 57
-Wayne Rooney: Goli 43 Mechi 99

No comments:

Post a Comment