Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 7, 2014

MEDIA DAY BONAZA KUFANYIKA DESEMBA


TASWA kila mwaka inaandaa bonanza la vyombo vya habari linalojulikana kama Media Day Bonanza, ambalo hushirikisha wadau mbalimbali kutoka vyombo vya habari.
 
Lengo la bonanza hilo ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.
 
Lakini  mwaka huu bonanza hilo limechelewa kutokana na na suala la wadhamini ambao awali TASWA ilikubaliana nao, lakini baadaye walisema wamepata matatizo ya kifedha.
 
Hata hivyo kutokana na umuhimu wa bonanza hilo, uongozi wa TASWA umezungumza na wadau wengine na mazungumzo hayo yanaendelea ili Media Day Bonanza ifanyike mwezi ujao likiwa ni maalum kwa ajili ya kufunga mwaka 2014.
 
Tunajua maswali kuhusu Media Day yamekuwa mengi pengine kuliko majibu, pia wasiwasi kwa baadhi yenu ni mkubwa kuliko uhakika, lakini tunawahakikishia mambo yanaenda vizuri na ni imani yetu yanakaribia kuiva.
 
Kwa hili la Media Day, tuliona ni bora tukawie kuliko kuvurunda. Tusikimbie kwa kasi bila kutazama tuendako. Tutambae, lakini macho njiani na mbele tunakoelekea na hiyo ndiyo dhamira yetu.
 
Ahsanteni,

No comments:

Post a Comment