Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani |
Bondia Iddi Piyalali akiwa na mkanda wa ubingwa wa Kanda ya Mashariki
Bondia Iddi Pialali
Bondia Iddi Pialali |
Bondia Hashimu Zuber kushoto
akipambana na Ally Mahiyo wakati wa mpambano wao uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo mkowa wa Pwani, Zuber alishinda kwa pointi
wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi wakifuatilia mchezo huo uliopigwa siku ya jumatatu kiwangwa bagamoyo mkoa wa pwani
Bondia Ally Bugingo kushoto akimtupia konde Twalibu Tuwa wakati wa mpambano wao Bugingo alishinda kwa pointi
Said Yazidu akiongea na mashabiki wakati wa mpambano huo
BAADHI YA WATU AMBAO WALIKOSA KUINGIA UKUMBINI KWA KUTOKUWA NA PESA WAKIPIGA CHAPO KWENYE DIRISHA
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Iddi Pialali mwanzoni mwa wiki
hii aliwainua mikono juu wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani
baada ya kunyakuwa ubingwa wa kanda ya mashariki kwa kumtwanga kwa K,O raundi ya tano bondia Fadhili Mkundi
Pambano huo uliofanyika siku ya jumatatu ulikuwa na shamrashamra nyingi tangia mwanzoni mwa mchezo huo ambapo watu walifulika kuona ndonga zikipigwa Kiwangwa mpambano huo wa ubingwa ulianza mnamo saa 4 na dakika 20 usiku
Huku mashabiki wakimshangilia Pialali kwa furaha mwanzo mwisho raundi ya kwanza ilianza kwa mashambulizi ya kutupiana makonde ya uku na kule ambayo yaliwavutia sana wakazi wa kiwangwa ilipofika raundi ya tatu mashambulizi yakawa kwa upande mmoja ambapo Pialali alibadilisha mchezo kwa kupiga ngumi za tumbo yani juu na chini kufika raundi ya tano Pialali aliongeza mashambulizi hayo kwa kasi na kumfanya refarii wa mpambano huo Pembe Ndava kumuhesabia mpinzani ambaye alikuwa akivuja damu puani na mdomoni ambapo mpinzani huyo alisalimu amri na Pialali kuibuka kidede kwa kushinda K,O raundi ya tano.

Kabla ya mpambano huo kulikuwa na
mapambano ya utangulizi yaliyowakutanisha mabondia Hashimu Zuber
aliyempiga kwa pointi Ally Maiyo na Ally Bugingo alimsambalatisha kwa
pointi Twalibu Tuwa
Mwisho wa mchezo huo promota wa mpambano huo Bernard Mwakyusa amewahaidi wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo kuwa atapeleka burudani ya masumbwi mara kwa mara kwa kuwa sasa kuna bingwa anayetambulika rasmi katika tasnia ya masumbwi nchini

No comments:
Post a Comment