Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 28, 2014

23 KUGOMBEA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA 2014 (FIFA BALLON d’Or)

JUMANNE OKTOBA 28, FIFA yatangaza Listi ya awali ya Wagombea 23 wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon d’Or, kwa Mwaka 2014 miongoni mwao yumo Cristiano Ronaldo ambae alitwaa Tuzo hii Mwaka Jana.
Mwaka 2013, Ronaldo anaechezea Real Madrid, alitwaa Ballon d’Or na kuvunja wimbi la Lionel Messi la kutwaa Tuzo hiyo kwa Miaka Minne mfululizo.

Majina hayo ya Wagombea 23 yameteuliwa na Kamati ya Soka ya FIFA ikishirikiana na Wataalam kutoka Jarida la France Football ambao ndio Waasisi hasa wa Ballon d’Or.
Kuanzia Mwaka 2010, France Football waliungana na FIFA na kuziunganisha Tuzo za Ballon d’Or pamoja na ile ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na kuitwa FIFA Ballon d’Or.

Listi hii ya Wagombea 23 inatarajiwa kupunguzwa hadi Wachezaji Watatu ifikapo Desemba na hao ndio watakaoingia Fainali ambayo Mshindi wake atatokana na Kura za Wanahabari wa Soka maalum, Makocha wa Timu za Taifa Duniani na Makepteni wa Timu hizo.
Mshindi wa FIFA Ballon d’Or kwa Mwaka 2014 atatangazwa hapo Januari 12, 2015 huko Zurich, Uswisi kwenye Kongresi ya FIFA, iitwayo Zurich Kongresshaus.
Angel Di Maria ni moja ya Wachezaji 3 walioteuliwa kugombea nafasi hiyo wanaocheza katika Ligi kuu England. Eden Hazard na Yaya Toure wamo ndani ya 23 katika Listi hiyo.

LISTI YA WAGOMBEA 23 WA   TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA 2014 (FIFA BALLON d’Or).
1. Gareth Bale (Wales)
2. Karim Benzema (France)
3. Diego Costa (Spain)
4. Thibaut Courtois (Belgium)
5. Cristiano Ronaldo (Portugal)
6. Angel Di Maria (Argentina)
7. Mario Goetze (Germany)
8. Eden Hazard (Belgium)
9. Zlatan Ibrahimovic (Sweden)
10. Andres Iniesta (Spain)
11. Toni Kroos (Germany)
12. Philipp Lahm (Germany)
13. Javier Mascherano (Argentina)
14. Lionel Messi (Argentina)
15. Thomas Mueller (Germany)
16. Manuel Neuer (Germany)
17. Neymar (Brazil)
18. Paul Pogba (France)
19. Sergio Ramos (Spain)
20. Arjen Robben (Netherlands)
21. James Rodriguez (Colombia)
22. Bastian Schweinsteiger (Germany)
23. Yaya Toure (Côte d’Ivoire)

No comments:

Post a Comment