Nyota
kinda wa Liverpool Suso ameripotiwa kukubali kujiunga na kigogo cha
soka nchini Italia AC Milan kwa uhamisho wa kudumu huku swali likisalia
kuwa ni lini mchezaji huyo mhispania kijana ataelekea Rossoneri.
Suso,
ambaye amekuwa katika kikosi cha kwanza cha Liverpool mara 14 alijiunga
Anfield
mwaka 2010, amekubali kuingia kandarasi ya miaka minne mkataba wenye
thamani ya pauni £1.2 kwa mwaka hii ikiwa ni kwa mujibu wa habari kutoka
nchini Italia.
Kijana
huyu raia wa Hispania amekuwa mchezaji huru tangu kumalizika kwa
mkataba msimu uliopita huku taarifa zaidi zikisema kuwa Milan
wanajipanga kukamilisha usajiliwa kiungo huyo mshambuliaji mwezi
Januari.
No comments:
Post a Comment