Sir
Alex Ferguson akizungumza na Carlo Ancelotti na Arsene Wenger katika
mkutano wa makocha mjini Nyon MKUTANO wa mwaka wa makocha wa kiwango cha
juu umeanza jana jumatano na kumalizika leo, makao makuu ya UEFA, mjini
Nyon, Uswizi.
Kocha wa zamani wa Manchester United,
Sir Alex Ferguson alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo akiwa kama balozi wa
makocha wa UEFA , wakati naye Rais Michele Platini alikuwepo. Ferguson
alinaswa na kamera akitaniana na aliyekuwa mpinzani wake mkubwa Arsene
Wenger, wakati bosi wa Manchester City, Manuel Pellegrini naye alikuwepo
katika tukio hilo. Wakizungumzia mchezo mzuri: Rais wa UEFA Michele Platini akizungumza na Ancelotti na Ferguson leo alhamisi. Picha ya pamoja ya makocha katika makao makuu ya UEFA leo nchini Uswizi. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akiwa amekaa na kocha wa zamani wa Stamford Bridge, Carlo Ancelotti
Mourinho akizungumza na waandishi wa habari nje ya makao makuu ya UEFA leo. Hata hivyo, kocha wa mashetani wekundu, Manchester United, Louis van Gaal - ambaye ni mshindi wa Bundesliga, La Liga na Eredivisie - hakuwepo katika mkutano huo kwasababu timu yake haishiriki michuano ya UEFA mwaka huu.
Louis van Gaal hakuhudhuria mkutano huo.
No comments:
Post a Comment