Mchezo huo wa nusu
fainali ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika itachezwa
katika Uwanja wa Setif maarufu kwa jina la Mei 8, 1945. Hii itakuwa
mara ya pili kwa timu hizo kukutana ambapo mara ya kwanza ilikuwa katika
mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ambapo Mazembe
walifanikiwa kutoa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
huku wakiwatandika Setif kwa mabao 4-2 katika mchezo wa marudiano
uliochezwa jijini Lubumbashi.
Setif ilishindwa kufurukuta katika kundi B
walilokuwepo baada ya kuburuza mkia, wakati Mazembe waisonga mbele
mpaka hatua ya nusu fainali mpaka fainali na baadae kuja kufungwa na CS
Sfaxien ya Tunisia kwa jumla ya bao 1-0 na kuibuka bingwa wa michuano
hiyo. Mchezo mwingine wa nusu fainali unatarajiwa kuchezwa kesho jijini
Kinshasa ambapo AS Vita watakuwa wenyeji wa Sfaxien.
No comments:
Post a Comment