Orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi katika ligi kuu ya soka Italia Seria yatolewa Teves nyuma ya De Rossi
De Rossi kinara kwa malipo ya pauni 77,000
Nyota wa Juventus Paul Pogba (kulia) anapata chini ya kiwango cha juu cha mshahara wa juu katika Seria A
Wachezaji wanaolipwa fedha nyingi nchini Italia katika Serie A wamewekwa bayana na mishahara hiyo imewashangaza baadhi ya watu.
Mmoja
wa wachezaji wenye vipaji Paul Pogba, anapokea kiasi cha pauni £23,000
kwa wiki kwa mabingwa wa Italia Juventus wakapo ambapo kiasi cha juu
kabisa cha ulipwaji wa mishahara kikiwa ni £77,000 akiwa ni kiungo wa
Roma Daniele de
Rossi.
Viwango
hivyo vya mishahara vilivyotajwa kupitia gazeti maarufu la 'Gazetta
dello Sport' pia vimeonyesha kuwa kiwango cha fedha za jumla za
mishahara kimeshuka kwa mara nyingine.
Nyota
wa Napoli Gonzalo Higuain na mshambuliaji wa zamani katika ligi kuu ya
England (Premier League) Carlos Tevez ameungana na De Rossi katika
orodha ya wachezaji watatu wa juu kimshahara huku Ashley Cole
aliyejiunga na Roma akitokea katika klabu ya Chelsea msimu wa kiangazi
amekatwa mshahara wake kwa kiasi kikubwa katika Serie A baada ya
kukubali mshahara wa pauni £35,000 kwa wiki.
Mchezaji
mwingine ambaye ameshuka kwa malipo kiangazi hii ni mshambuliaji wa
zamani wa Chelsea Fernando Torres, ambaye atakuwa akipokea pauni £61,000
kwa wiki katika klabu ya AC Milan ikiwa ni kiwango kilicho poromoka kwa
kiwango kikubwa kutoka katika malipo ya pauni £175,000 kwa wiki
alipokuwa huko London ya kaskazini.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wanao lipwa zaidi katika ligi kuu ya nchini Italia Serie A
No comments:
Post a Comment