Rais wa Simba Evance Aveva akielezea jambo wakati wa mkutano mkuu wa wanachama wa klabu Simba uliofanyika Bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. |
Hii ni sehemu ya wanachama wa klabu ya Simba waliohudhuria mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam |
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba Dr Damas Ndumbaru akizungumza wakati wa mkutano huo |
Sehemu ya wanachama wa klabu ya Simba wakifuatilia kwa makini mkutano mkuu wa kwanza wa klabu yao chini ya Rais wa kwanza wa klabu hiyo Evance Aveva |
Mkutano mkuu wa klabu ya Simba uliofanyika leo katika bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay umewafuta uanachama wanachama 72 wa klabu hiyo kutokana na kile kilicho elezwa kuwa ni kuelekea mahakama za kiraia kupinga uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika mwezi Juni.
Pamoja na wanachama hao mwingine aliyefutwa uanachama wake ni aliyewahi kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo Michael Richard Wambura ambaye naye amefutwa uanachama wake kutokana na kuipeleka Simba mahakamani mwaka 2010 na kungua file namba 100 kupinga jina lake kuenguliwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi akiwa na mwenzake Mtemi.
Akiongea hii leo mbele ya wanachama zaidi ya 800 waliohudhuria mkutano huo, Rais Aveva ameonyesha kushangazwa kwake na uongozi wa Simba wa wakati ule kushindwa kuwaondoa uanachama akina Wambura kitu ambacho uongozi wake mara baada ya kuingia madarakani umelifanya baada ya kupokea taarifa ya TFF ya kwamba kitendo kilichofanywa na wanachama hao kilikuwa hakikubaliki na kwamba endapo uongozi mpya untashindwa kuwaondoa wanachama hao basi Simba Sports Club wangefutwa uanachama wa TFF.
Aveva pamoja na kuwasomea wanachama hao ibara ya 55 ya katiba ya Simba ambayo inakataza mpira kwenda mahakamani, pia aliwahoji wanachama wa klabu hiyo ambao kwa kauli moja walikubaliana kuwafuta uanachama wanachama hao.
No comments:
Post a Comment