Meneja wa Manchester
United Louis van Gaal amesema kipigo cha wiki iliyopita kutoka ka Swansea
katika ligi kuu ya Barclays Premier hakipaswi kumgeuza yeye kuwa shetani mbele ya mashabiki wa klabu hiyo.
Mwanzo
wa kazi wa Van
Gaal katika klabu ya United ulikuwa mbaya wiki iliyopia na watakuwa
wakielekea katika mchezo ujao Sunderland jumapili wakiwa na majeraha
ambayo mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakihoji ubora wa kikosi chao
kabla ya kukabiliana na Sunderland.
IKiwa
tayari imefahamika kuwa mshambuliaji Danny Welbeck huenda akaondoka
kikosi, presha imepanda kwa Van Gaal ndani ya Old Trafford.
Anajipa moyo: Louis van Gaal amewataka mashabiki wa Manchester United kuwa na subira
Wakati
mgumu: Wayne Rooney na Co watakuwa wanatarajia kurejesha matumaini
kufuatia kupoteza katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Swansea
Van
Gaal amesema
'Siku zote iko namna hiyo, kwa wiki mbili zilizopita nilikuwa mfalme wa Manchester na sasa nimekuwa shetani wa Manchester.
"Dunia ya mpira na hususani vyombo vya habari katika mpira duniani ndivyo walivyo.
'Nadhani
mashabiki wa Manchester wana akili na nimekuwa nikisema katika mikutano
yote ya vyombo vya habari nchini Marekani kuwa miezi mitatu ya mwanzo
itakuwa migumu kwa wachezaji na mashabiki.
'Nimelisema hilo kwa mtendaji mkuu Ed Woodward na Glazers kuwa hivi ndivyo ilivyo.
'Wameniajiri mimi kwa kutokana na Filosofia yangu na si kwasababu ya uzuri wangu.
Mimi ni mtu mzuri lakini hiyo siyo sababu ya mimi kuwepo hapa.
Rooney atakuwa akiongoza kikosi cha Manchester United watakapo kuwa safarini Sunderland Jumapili
'Sijaajiriwa
ili nifukuzwe (I’m
not hired to be fired). NImeajiriwa kujenga kikosi, mchakato huo
unahitaji muda, naingiza filosofia yangu katika klabu na hiyo ni ngumu
kwasababu natakiwa kutoa maelezo ya kutosha.
No comments:
Post a Comment