Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 5, 2014

Usajili Ulaya: Newcastle yatua kwa Ferreyra, Inter Milan wana milioni 10 kwa ajili ya Gary Medel, Lampard atua Manchester City, Juventus wawajibu Man United kwa Nani na Hernandez wakati Liverpool wanakamilisha kwa ajili ya Manquillo wa Atletico Madrid..........


Mshamuliaji Facundo Ferreyra

Newcastle United imemsajili mshambuliaji wa  Shakhtar Donetsk Facundo Ferreyra kwa mkopo wa msimu mzima.

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 ni miongoni mwa wachezaji sita wa Shakhtar ambao mwezi uliopita walitangaza kutokurejea tena Donetsk kutokana na vita nchini Ukraine.

Ferreyra anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na timu hiyo  majira haya ya kiangazi na kuna uwezekanao wa kununuliwa kwa minajili ya moja kwa moja baada ya msimu kumalizika.

Meifungia Shakhtar jumla ya magoli 22 msimu uliopita tangu ajiunge nayo kwa umaihso uliogharimu kiasi cha pauni £6m akitokea Velez Sarsfield mwezi Julai 2013.

Siku ya Ijumaa , Pardew alikanusha taarifa za kutaka kumsajilia mshambuliaji wa Queens Park Rangers Loic Remy, ambaye aliifungia timu yake jumla ya magoli 14 katika jumla ya michezo 27 aliyoichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita.

Remy mweye umri wa miaka 27, alitarajiwa kujiunga na Liverpool kabla ya mpango huo kuvunjika na Alan Pardew amethibitisha kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa mara ya pili

Gary Medel: Inter Milan yakutana na Cardiff City wakiwa na £10
Gary Medel kung'oka Cardiff kiangazi hii?
Inter Milan imekutana na Cardiff City wakiwa na kiasi cha pauni milioni £10 mkononi kwa lengo la kuulizia uwezekano wa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Chile Gary Medel.

Kinachosubiriwa ni  kitengwa kwa muda ili vilabu hivyo kuketi kabla ya kufikia makubaliano.

Taarifa zinasema kuwa Cardiff City iliwahi kukataa mpango mwingine wenye thamani ya pauni milioni £5 kwa ajili ya kiungo Jordon Mutch kutoka kwa Queens Park Rangers.

Cardiff inajipanga kufanya usajili wa wachezaji wanne kabla ya mchezo wa ufunguzi wa ligi ndogo ya England maarufu kama ‘Championship’ dhidi ya Blackburn Rovers itakayopigwa Agosti 8.

Medel ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya usajili ya Cardiff ya pauni milioni £11 ambapo alijiunga nao akitokea Sevilla Agosti mwaka jana.

Mpaka sasa meneja Ole Gunner Solskjaer amewasajili kiangazi hii nyota hawa wafuatao
    Javi Guerra – mshambuliaji akitokea Real Valladolid (huru)
    Guido Burgstaller – Kiungo akitokea Rapid Vienna (huru)
    Federico Macheda – Mshambuliaji akitokea Manchester United (huru)
    Adam Le Fondre – Mshambuliaji kutoka Reading (kwa mkataba uliohifadhiwa)
    Kagisho Dikgacoi – Kiungo kutoka Crystal Palace (huru)

Frank Lampard: Bosi wa Man City Pellegrini athibitisha kumsajili kwa mkopo Lampard mpaka Januari.
Hatimaye Lampard anarejea ligi kuu ya England
Frank Lampard atajiunga na Manchester City kwa mkopo akitokea New York City FC mpaka January, hizi zikiwa ni taarifa zilizothibitishwa na meneja Manuel Pellegrini.

"kuanzia wiki ijayo, Jumatano ataanza kufanya kazi na sisi na takuwa na sisi mpaka January," Pellegrini amekaririwa katika mkutano na wana habari hiyo jana.

"Anafanya kazi na kikosi. Atakuwa akisaka nafasi."

Kiungo huyo mweye umri wa miaka  36 alijiunga na New York City mwezi uliopita kwa mkataba wa miaka baada ya kuachiliwa na Chelsea.

Manchester City inajipanga kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa England kwa ajili ya Ligi kuu na michuano ya vilabu bingwa Ulaya.

"Anajua tuna timu nzuri, tuna wachezaji wengi katika nafasi yake ya kiungo, nay eye anaongezeka" Amekaririwa Pellegrini akisema muda mfupi baada ya kichapo cha mabao 5-4 cha penati kutoka kwa Olympiakos mchezo wa maandalizi ya msimu.

Lampard amekuwa na mkongwe mwenye hadhi kubwa katika klabu ya Chelsea kufuatia miaka 13 ya kuitumikia Stamford Bridge, ambako amefunga jumla ya magoli 211 katika jumla ya 649 aliyoichezea Chelsea na kumfanya kuwa mfungaji mwenye rekodi ya juu kabisa ya klabu hiyo.

Juventus wajibu maombi ya Manchester United ya Vidal kwa Nani na Hernandez
Luis Nani ndani ya majaribu ya Juve

Juventus  wameanza kuwafuatialia nyota wawili wa Manchester United Luis Nani na Javier Hernandez ikiwa ni kujibu mapigo ya safari ya nyota wa kimataifa wa Chilean Arturo Vidal.

Vidal amekuwa akihusishwa kuondoka kwa bibi kizee cha Turini kwa pauni milioni £40 na kujiunga na Mashetani wekundu kiangazi hii na inaaminika kuwa tayari United wamekuwa wakiwasumbua mabingwa hao wa Italia juu ya Vidal ambaye inasemekana wamegomea.

Kwa mujibu wa taarifa zilizo ripotiwa katika gazeti moja la nchini Italia la Corriere dello Sport, ni kwamba Juventus imeahirisha kumuuza kiungo huyo mwenye kipaji cha hali ya juu kwa United huku nao wakianzisha mpango mpya wa kuwasajili Luis Nani na 
Javier Hernandez anatakiwa na Juventus
Hernandez ambao kwasasa wamekuwa hawana nafasi Old Trafford.

Thamani ya Vidal imezidi kuongezeka baada ya kuonyesha soka ya hali ya juu katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil na tangu wakati huo amekuwa akihusishwa na kuelekea ligi kuu ya England.

Vidal mwenye umri wa miaka 27 ambaye alijiunga na Juventus akitokea Bayer Leverkusen kiangazi 2011, na mwaka jana aliongeza mkataba wake na na klabu hiyo.

Liverpool wanaendelea kukomba wachezaji kuelekea msimu mpya wa ligi mara hii watua Atletico Madrid
Mlinzi wa kushoto wa Atletico Madrid Javier Manquillo kujiunga na Liverpool
Liverpool wanakaribia kuingia mkataba wa mkopo wa miaka miwili na mlinzi wa kushoto wa Atletico Madrid Javier Manquillo.

Brendan Rodgers amekuwa akiendelea kuimarisha kikosi chake kwa kufanya usajili kila kukicha, ambapo kiangazi hii amefanya usajili wa wachezaji kadhaa nyota na sasa akitarajia kumpata mlinzi huyo wa Madrid.

Adam Lallana, Rickie Lambert na Dejan Lovren wamesajiliwa wakitokea Southampton,  wakati ambapo Emre Can, Divock Origi na Lazar Markovic wakitoka nje ya England.

Kwa mujibu wa gazeti la Telegraph, ni dhahiri kuwa Manquillo ataonekana Anfield msimu ujao ambapo mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 20 anatarajiwa kuelekea Merseyside hapo kesho Jumatatu kwa ajili ya kipimo cha afya.

Mpango huo ambao unatarajiwa kukamilika siku chache zijazo, umeipa nafasi Liverpool kumsajili mlinzi huyo moja kwa moja kwa thamani ya pauni milioni £5 msimu ujao wa usajili wa kiangazi.

Manquillo ni mmoja kati ya walinzi ambao Rodgers anataka amekuwa akitaka kuwasajili huku pia mazungumzo yakiendelea na klabu ya Sevilla kwa ajili ya mlinzi mwingine wa kushoto Alberto Moreno.

No comments:

Post a Comment