Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 5, 2014

WACHEZAJI WA ALGERIA WATOA POSHO ZAO KWA WATU WA GAZA.


MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Algeria Islam Slimani amebainisha kuwa kikosi kizima cha nchi hiyo kinatarajiwa kutoa msaada wa posho zao kwa watu wa Gaza. Baada ya kutolewa katika hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Dunia na Ujerumani huku wakuonyesha kiwango bora na kuwalazimisha wapinzani wao kwenda katika muda wa nyongeza kabla ya kufungwa mabao 2-1. Timu ilirejea nyumbani wakiwa mashujaa na wachezaji wameamua kutoa posho zao kwa wale ambao wanazihitaji zaidi. Hatua hiyo ya Algeria imekuja huku wawakilishi wengine wa Afrika katika michuano hiyo kama Ghana, Nigeria na Cameroon kukumbwa na msuguano katika kambi zao kutokana na posho hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuenguliwa mapema.

No comments:

Post a Comment