Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 2, 2014

LALLANA ATUA RASMI LIVERPOOL.

KIUNGO mahiri Adam Lallana amekamilisha uhamisho wake wa paundi milioni 25 kutoka klabu ya Southampton kwenda Liverpool. 
Lallana mwenye umri wa miaka 26 anakuwa mchezaji wa pili kusjailiwa na meneja wa Liverpool Brendan Rodgers katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi akiungana na mchezaji mwenzake Rickie Lambert kwa mkataba wa muda mrefu. 
Kiungo huyo ambaye aliiwakilisha Uingereza katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil ameichezea Southampton mechi 265. Lallana ambaye alifaulu vipimo vya afya mwishoni mwa wiki iliyopita amesema anafuraha kubwa kuanza ukurasa mpya katika kazi yake ya kusakata kabumbu katika klabu hiyo ya kipekee ya Liverpool. Lallana atakuwa akivaa fulana yenye namba 20 mgongoni akiwa na Liverpool.

No comments:

Post a Comment