Divorc Origi aliisaidia Ubeligiji kufika awamu ya 16 bora nchini Brazil |
Lakini pia amesema watajadialiana mambo kadhaa
pamoja na timu zingine ambazo zinataka kumsajili Origi ambaye
aliiwakilisha Ubelgiji kwenye mashindano ya kombe la dunia nchini
Brazil.
Mbali
na Liverpool timu zingine za ligi kuu ya England ambazo zimeonyesha nia
ya kumsajili Origi ni Tottenham Hotspur na Arsenal lakini hawajataja
kiasi cha fedha mbazo wako tayari kutoa.
Akizungumza hii leo kutoka Ubelgiji, Okoth, ambaye alihudhuria mashindano ya kombe la
dunia anasema bado anamsubiri kijana wake arudi kutoka Ubelgiji kisha azungumze naye.
''Yeye ni mtu mzima mwenye uwezo wa kujiamulia
mengine. Kuna timu kutoka Ujerumani, Italia na Hispania ambazo
zimewasiliana nasi kupitia wakala wao.Itabidi tuchunguze uzito wa timu
hizo na makocha wanaozifunza,’’ alisema babake Origi.
'Klabu ya kumkuza Origi'
Katika mashindano hayo
yanayomalizika Jumapili hii, Origi aliiwezesha Ubelgiji kufuzu kwa
raundi ya pili alipofunga bao na kuilaza Urusi 1- 0. Aliingia katika
kipindi cha pili na kuchukua nafasi yake Romelu Lukaku.
''La mhimu ninalotaka ni ajiunge na klabu
itakayomkuza na apate fursa nzuri ya kujiendeleza. Sitafurahia ajiunge
na klabu ambayo hatapata muda wa kutosha wa kucheza hata kama pesa ni
nyingi. Siangalii tu pesa lakini nalenga mbele kimchezo.Anaweza kujiunga
na klabu inayotoa pesa nzuri za kuhama lakini singetaka mara tu akivuka
aanze kujuta kama hachezi mara kwa mara.’’
Kwa sasa Origi anaichezea Lille ya Ufaransa lakini anasema lengo lake kubwa ni kushiriki ligi kuu ya England.
Okoth anasema licha ya kwamba yeye ni shabiki wa
Liverpool watazungumzia zaidi mambo mengine na Origi akirudi Ubelgiji
kutoka Brazil ambako aliiwakilisha taifa lake alikozaliwa na kufurahisha
wengi wakiwemo mashabiki wa Kenya ambao baadhi yao walibubujikwa na
machozi Ubelgiji ilipong’olewa na Argentina kwenye mechi ya robo-fainali
ambayo walipoteza kwa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment