Bondia Zumba Kukwe kushoto akioneshana umwamba na Josef Njelekela wakati wa mpambano wao waliotoka droo
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
kushoto akimpongeza khalid chokolaa baada ya kuibuka mshindi katika
mpambano wake
Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ubingwa wa UBO umekosa
kutangazwa mshindi mbele ya mashabiki baada ya vurugu kubwa kutokea
katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Dar es salaam jana.
uUingwa huo uliokuwa ukigombaniwa na
mabondia Said Mbelwa na Karama Nyilawila alishindikana kupatikana
mshindi baada ya raundi ya nane bondia Karama kumpiga kichwa Mbelwa cha
wazawazi na kusababisha Mbelwa kuhamaki kwa kulipiza kisasi na kumsukuma
nje pia kumrukia wakati alipotoka nje ya ulingoni mpambano huo
wa raundi kumi ulijikuta ukishia kwa raundi nane
Waamuzi pamoja na majaji walikimbia ukumbini wakiwaacha mashabiki bila kuleta majibu ya mpambano
huo hata hivyo Mbelwa alirudi ulingoni kwa ajili ya kuendelea kupambana
na mpinzani waka alikimbia moja kwa moja kutokana na kuona
ngumi za mtaani ndizo zinashika kasi.
wakati huohuo bondia Mada Maugo alimpiga mwenzake Thomas Mashali kwa ngumi tatu mfululizo
bila kufata sheria ambapo ni kinyume
na taratibu za mchezo wa masumbwi duniani. Mabondia hao wote
walionekana wamelewa walishindwa kuelewana mbele ya promota Ally Mwazoa
Katika mapambano ya utangulizi
yaliyochezwa bondia Khalid Chokoraa ambaye ni mwanamuziki
alimpiga kwa KO ya raundi ya kwanza Abdul Manyenza na Mwaite Juma
alimpiga Athumani Rashid wa Tanga kwa pointi wakati Selemani Galile
alipigwa kwa pointi na Abdalah Pazi
No comments:
Post a Comment