Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, May 25, 2014

CECAFA NILE BASIN: MBEYA CITY YAANZA VYEMA! YAIFUNGA BAO 3-2 ACADEMIE TCHITE YA BURUNDI


RIPOTI toka huko Khartoum, Sudan zimesema Wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye Michuano ya CECAFA NILE BASIN, Mbeya City, Leo hii wameanza vyema Masindano hayo kwa kuichapa Academie Tchite ya Burundi Bao 3-2 kwenye Mechi ya KUNDI B.Kwenye Mechi hii, Bao za Mbeya City zilifungwa na Paul Nonga, Mwegane Yeya na Themi Felix.
Hapo Jana, Timu ya Zanzibar, Polisi, ilichapwa Bao 3-0 na Wenyeji Al-Merreikh ya Sudan.
Kufuatia kujitoa kwa Timu 5 katika Dakika za mwisho, CECAFA iliamua kubadilisha Makundi na Ratiba ya Mashindano haya.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa CECAFA, Rogers Mulindwa, Timu zilizojitoa ni pamoja na Wageni Waalikwa maalum, Klabu za Egypt Al Masry na.Arab Contractors.

Nyingine ni Elman ya Somalia na Klabu ya Sudan, Hey Al Arab.
Hali hiyo imefanya Timu kubakia 11 na Makundi kuwekwa kuwa Matatu.


RATIBA/MATOKEO
Ijumaa Mei 23

Victoria University (Uganda) 1 - 0 Malakia (South Sudan)
Al-Merreikh [Sudan] 3 - 0 Police [Zanzibar]
Al-Shandy [Sudan] 2 - 1 Dkhill [Djibouti]

Jumamosi Mei 24
Mbeya City [Tanzania] 3 Academie Tchite [Burundi] 2
AFC Leopards [Kenya] v Etincelles [Rwanda]
MAKUNDI
KUNDI A

-Polisi [Zanzibar]
-Victoria University Uganda]
-Malakia [South Sudan]
Al Merreikh [Sdan]

KUNDI B
-Mbeya City [Tanzania Bara]
-AFC Leopards [Kenya]
-Academie Tchite [Burundi]
-Enticelles [Rwanda]

KUNDI C
-Defence [Ethiopia]
-Dkhill FC [Djibouti]
-Al Shandy [Sudan]

No comments:

Post a Comment